Akitoa hotuba yake ya Ijumaa mbele ya zaidi ya Mahujaji nusu millioni katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al-Sudaisi amesema: "Hapa ni mahala patakatifu na wakati wa kusulushisha migogoro ambayo imeuletea ummah masaibu mengi. Hatupaswi kuwa na migongano. Moja ya matatizo makubwa ni Palestina. Ndugu zetu Wapalestina wanaumia kutokana na ukosefu wa uadilifu na mzingirio wa utawala ghasibu wa Israel na vile vile kutokana na malumbano na migongano miongoni mwao.
Imamu wa Msikiti Mtukufu wa Makka Sheikh Abdulrahman as-Sudaisi amewakaribisha mahijaji katika mji wa Makka na kuitaja Hija kuwa ni safari ya tauba na uchamungu. Ametoa wito kwa mahujaji kujiepusha na madhambi. "Usalama wa mahujaji uko mikononi mwa Allah SWT. Utukufu wa misikiti miwili mitakatifu hauwezi kuvurugwa na migogoro au harakati za walio na misimamo mikali", amenukuliwa na gazeti la Arab News. 327464