Aidha amewatakia mahujaji wote Hija makbuli kwa Mwenyezi Mungu sw.
Gazeti la kila siku la Lebanon la al-Mustaqbal limemnukulu Sheikh Qabbani akimshukuru pia Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia kwa kuongeza idadi ya Mahujaji wa Lebnon mwaka huu. Vilevile ametoa shukrani zake kwa Saad Hariri mkuu wa mrengo wa al Mustaqbal kwa juhudi zake kuhusiana na suala hilo.
Katika upande mwingine, Daru Ifta ya Lebanon imetoa taarifa rasmi na kutangaza kuwa: 'Kwa mujibu wa sheria, siku ya Jumamosi 29 Novemba ndio iliyokuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul Hija mwaka 1349 Hijria Qamariya na kwa hivyo, Jumapili tarehe 7 Desemba itakuwa siku ya Arafa na Jumatatu tarehe 8 Desemba (nayosadifiana na 10 Dhil Hija) itakuwa siku ya Idul Adh-ha".328329