IQNA

Maonyesho ya vyaraka za maandishi ya mkono za Kiislamu za Maktaba ya Chuo Kikuu cha Bratislava

10:42 - December 08, 2008
Habari ID: 1717014
Maonyesho ya nyaraka za maandishi ya mkono za Kiislamu za Maktaba ya Chuo Kikuu cha Bratislava cha Jamhuri ya Slovakia yameanza leo Jumatatu katika majengo ya Maktaba ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mahusiano ya Umma ya Shirika la Nyaraka na Maktaba ya Taifa, sherehe za kutiwa saini hati ya ushirikiano kati ya shirika hilo na Maktaba ya Chuo Kikuu cha Bratislava zimefanyika hii leo Jumatatu katika majengo ya Shirika la Nyaraka na Maktaba ya Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo, Ali Akbar Ash'ari, Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nayeshughulikia masuala ya utamaduni ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Nyaraka na Maktaba ya Taifa la Iran na vilevile Profesa Taibour Targina, Mkuu wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Bratislava watatoa hutuba kuhusiana na umuhimu wa chuo kikuu hicho na maonyesho hayo. Nyaraka za kale zitakazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na nuskha 393 ziliozoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, 117 za Kituruki na 88 za Kifarsi. Zaidi ya nuskha 490 ya hizo ni za chapa ya kale na tayari zimesajiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco, mwaka 1997. Nuskha adimu na za pekee zikiwemo za Abu Ali Sina na zilizotarjumiwa kwa lugha ya Kislovaki ni miongoni mwa nyaraka zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Bratislava iliyoasisiwa mwaka 1919 inahesabiwa kuwa maktaba muhimu zaidi ya Jamhuri ya Slovakia. Ina zaidi ya kopi milioni mbili na nusu na inategemewa sana katika nchi za Ulaya, Shughuli zote za Maktaba ya Taifa ya Slovakia zinafanyika katika maktaba hiyo. 331016
captcha