IQNA

Shirika la Nishati la Kiislamu kuasisiwa nchini Pakistan

10:20 - December 09, 2008
Habari ID: 1717408
Shirika la Nishati la Kiislamu litazinduliwa hivi karibuni nchini Pakistan kwa shabaha ya kuandaa uwanja wa kushirikiana nchi za Kiislamu katika sekta ya nishati.
Gazeti la Pakistan Daily limemnukuu Sayyid Mahdi Hussein, mmoja wa wajumbe wa tume ya kuandaa mipango ya kuasisiwa shirika hilo akisema kuwa, shirika hilo ambalo litabuniwa kwa minajili ya kuimarisha mazungumzo ya nchi za Kiislamu kuhusiana na kadhia ya nishati, kimsingi litaanza shughuli zake rasmi baada ya kupitishwa hati ya kubuniwa kwake. Ameendelea kusema, kuyasaidia mashirika ya nishati ya Iran yashiriki katika uendeshaji wa miradi ya nishati ya kieneo na vilevile kuzisaidia sekta binafsi za nchi za Kiislamu zishiriki katika miradi ya ustawi wa mafuta na gesi nchini Iraq, ni malengo mengine ya kubuniwa shirika hilo. Mahdi Hussein amemaliza kwa kusema, kwa kuwa wanachama katika shirika hilo, nchi za eneo zinaweza kushirikiana katika uwanja wa nishati na hivyo kuondoa kasoro na udhaifu wa nchi za Kiislamu katika uwanja huo. 331509
captcha