IQNA

Umoja wa Mataifa usitosheke tu kwa kutoa taarifa kuhusiana na kadhia ya Gaza

10:11 - December 09, 2008
Habari ID: 1717410
Rais Abdallah Swaleh wa Yemen amemtaka Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi za kumaliza mzingiro wa Ukanda wa Gaza na kutotosheka tu na kutoa taarifa zisizokuwa na uzito mkubwa katika kupunguza masaibu yanawapata wakazi wa ukanda huo.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Yemen, Rais Abdallah Swaleh amesema kwamba, hatua za kinyama zinazotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza zinakiuka maazimio na sheria zote za kimataifa. Amekosoa vikali siasa za kundumakuwili na upendeleo zinazotekelezwa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai za utawala haramu wa Israel na kumtaka Ban Ki Moon aingilie kati ili kupunguza machungu na masaibu yanayowapata wananchi wa Palestina na hasa wakazi wa Ukanda wa Gaza. Mwishoni, Rais Abdallah Swaleh amesikitishwa na kimya cha jamii ya kimataifa kuhusiana na mateso pamoja na jinai hizo zinazotelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Gaza. Amesema, utawala huo unazuia kuingizwa katika ukanda huo bidhaa za dharura kabisa za kibinadamu yakiwemo madawa, chakula, maji na umeme ilhali walimwengu wamekaa kimya bila ya kuchukua hatua yoyote ya kukabiliana na jinai hizo. Itakumbukwa kuwa, Ban Ki Moon ametoa taarifa akielezea wasiwasi wake kuhusiana na matatizo yanayowapata Wapalestina wakazi wa Ukanda wa Gaza na kuutaka utawala wa Kizayuni ujiepushe kuwazuia watoa misaada kuingia katika ukanda huo ili kuokoa maisha ya wahitaji wa misaada hiyo ya dharura. 331519
captcha