IQNA

11:07 - December 20, 2008
Habari ID: 1720542

Filamu ya Fitna yapigwa marufuku katika bunge la Ulaya

Mbunge katika bunge la Ulaya Gerard Batten amesema kuwa filamu inayokebehi matukufu ya Kiislamu ya Fitna iliyotengenezwa na mbunge wa Uholanzi mwenye misimamo ya kuchupa mipaka Geert Wilders imepigwa marufuku kuonyeshwa katika makao ya bunge la Ulaya mjini Strasbourg.

Gerard Batten amesema: Filamu ya Fitna ambayo ilipangwa kuonyeshwa katika bunge la Ulaya imepigwa marufuku na kwamba Geert Wilders amekwishapewa taarifa hiyo. Amesema kuwa uamuzi wa kupiga marufuku kuonyeshwa filamu hiyo umepasishwa na Baraza la Marais wa Bunge la Ulaya linalojumuisha Spika wa Bunge hilo na wakuu wa makundi ya kisiasa.
Hata hivyo Mbunge Gerard Patten amedai kwamba kupigwa marufuku filamu hiyo kuonyeshwa katika bunge la Ulaya kunakinzana na uhuru wa kujieleza. Mbunge huyo amesahau kwamba filamu hiyo inayotusi na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu imewakasirisha Waislamu bilioni moja na nusu kote duniani baada ya kuonyeshwa katika mtandao wa intaneti. 335361
captcha