IQNA

Kitabu cha "Madhehebu na Nchi" chatarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili

15:52 - December 22, 2008
Habari ID: 1721656
Kitabu cha al Madh-hab wal Watan (Madhehebu na Nchi) kilichoandikwa na Sheikh Hassan Saffar Imamu wa Ijumaa wa msikiti wa Qatif, Saudi Arabia kimetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili na kuchapishwa nchini Kenya.
Kitabu hicho ambacho kimepewa jina la Madhebu na Dini, kimetarjumiwa kwa Kiswahili na mtafiti wa masuala ya Kiislamu wa Kenya Khalfan Kiya.
Kitabu hicho kinakusanya mahojiano ya Sheikh Hassan Saffar na Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni na Masuala ya Kiislamu cha gazeti la al Madina linalochapishwa nchini Saudi Arabia. Mahojiano hayo yanajadili suala la uwiano na mfungamano kati ya madhehebu utaifa.
Kitabu hicho kinasisitiza kuwa hisia na imani za kimadhehebu za mtu hazipingani na hisia zake za kitaifa na kwamba kuipenda nchi ni sehemu ya imani. Sheikh Hassan Saffar anasisitiza kwamba, mtu anayeisaliti nchi yake huwa hana dini.
Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kiarabu mjini Beirut, Lebanon mwaka 2006 na chapa yake ya pili ilitolewa mwaka huu katika mji wa Qatif, Saudi Arabia.
Hadi sasa vitabu kadhaa vya Sheikh Hassan Saffar vimetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili ikiwa ni pamoja na "Masalafi na Shia, Hatua za Kujenga Uhusiano Bora Zaidi", "Imam Mahdi, Bishara ya Matumaini", "Ndoa, Malengo na Sheria Zake" na kadhalika. 336752

captcha