IQNA

Polisi wachunguza hujuma dhidi ya Msikiti nchini Uswidi

17:27 - September 24, 2025
Habari ID: 3481280
IQNA – Moto umeteketeza msikiti katika mji wa kusini wa Hultsfred, nchini Uswidi, usiku wa kuamkia Jumanne, na kuharibu kabisa jengo hilo.

Moto huo uliiacha jengo hilo katika hali ya magofu. Polisi wamesema kuwa wanachukulia tukio hili kama shambulio la uteketezaji kwa makusudi (arson), kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo.

Kulingana na Sweden Herald, moto ulianza Jumatatu usiku na kuenea haraka ndani ya jengo, ambalo awali lilikuwa kanisa kabla ya kubadilishwa kuwa msikiti.

“Hatufahamu jinsi moto ulivyoanza, lakini ulikuwa umeshika kwa nguvu ndani ya jengo,” amesema Michael Hesselgard wa idara ya uokoaji.

Hakuna majeraha yaliyoripotiwa, lakini jengo hilo limegeuka magofu.

“Jengo litakuwa limeharibiwa kabisa. Haliwezekani tena kutumika kwa kitu chochote,” aliongeza Hesselgard.

Vikosi vya uokoaji vilibaki eneo la tukio hadi asubuhi kuhakikisha moto umetoweka kabisa, kisha polisi walilizingira eneo hilo ili kuanza uchunguzi.

Msemaji wa polisi Patric Fors amethibitisha kwamba kesi hii inachunguzwa kwa shaka ya uteketezaji kwa makusudi.

“Aina ya uchunguzi imewekwa hivyo kwa sababu hatujui ni kwa nini moto umeanza kuwaka,” alisema.

3494731

captcha