Walipata nafasi ya kufika fainali baada ya kuonyesha utendaji bora katika raundi za awali. Kitengo cha Mambo ya Qur’ani cha Shirika la Awqaf au Wakfu na Huduma za Hisani kimeendesha raundi za miji na mikoa kwa ushirikiano na maofisi ya Awqaf katika mikoa mbalimbali nchini humo.
Hatua ya fainali imepangwa kufanyika mjini Sanandaj, katika mkoa wa magharibi wa Kurdistan, kuanzia tarehe 18 hadi 29 Oktoba.
Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yanayoandaliwa na Shirika la Awqaf, ndiyo mashindano makubwa zaidi ya Qur’ani nchini , yakivutia washiriki kutoka pande zote za nchi kushindana katika nyanja mbalimbali.
Mashindano haya ya kila mwaka, yanayochukuliwa kuwa tukio lenye heshima kubwa zaidi la Qur’ani nchini Iran, yanalenga kukuza maadili ya Kiislamu, kuimarisha elimu ya Qur’ani, na kusherehekea vipaji vya kipekee. Yanaandaliwa katika aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani, Tarteel, uhifadhi (hifdh), na Adhana. Washindi wakuu wataiwakilisha Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kote ulimwenguni.
3494729