IQNA

Tabu kubwa zaidi la picha za msikiti wa al Aqsa lazinduliwa

17:03 - December 22, 2008
Habari ID: 1721706
Tabu kubwa la picha za msikiti wa al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, limezinduliwa katika mji mtakatifu wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho zimehudhuriwa na waandishi na viongozi wa masuala ya utamaduni wa Palestina.
Kitabu hicho kimechapishwa na Idara ya Utafiti, Nyaraka na Upashaji Habari ya Quds.
Mwandishi wa kitabu hicho Muhammad Gosha amesema: Kitabu hicho kisichukuwa na kifani, kimekusanya habari zote na kamili kuhusu athari za Kiislamu za msikiti wa al Aqsa. Amesema: Kinabainisha umuhimu na nafasi ya kibla cha kwanza cha Waislamu.
Muhammad Gosha ameongeza kuwa, kitabu hicho kina kurasa elfu tatu na kimekusanya picha za athari na turathi za thamani za msikiti wa al Aqsa na za Kiislamu za mji mtukufu wa Quds. 336152

captcha