IQNA

17:25 - December 22, 2008
Habari ID: 1721711

Mayahudi wenye misimamo mikali wamvunjia heshima Mtume wa Uislamu

Kundi moja la Mayahudi wenye misimamo ya kufurutu mipaka limemvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad (saw) kwa kuandika maneno ya kudhalilisha kwenye kuta za msikiti wa al Bahr katika mji wa Yafa, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Yafa Ahmad Abu Ajwa ametoa taarifa akilaani uhalifu huo na amewataka Waislamu kujibu kitendo hicho kiuvu cha Mayahudi wabaguzi wenye misimamo ya kuchupa mipaka.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Waqfu na Turathi za al Aqsa pia amesema kuwa Waislamu waliokwenda kutekeleza swala ya asubuhi katika msikiti wa al Bahr wamekuta maandishi ya lugha ya Kiebrania yanayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na Waislamu kwenye kuta na milango ya msikiti huo.
Zaki Igbariya amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Mayahudi wenye misimamo mikali katika mji wa Yafa wamekuwa wakitekeleza mpango maalumu wa kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na kuchoma moto msikiti wa Hassan Bek na kuharibu makaburi ya Waislamu wa mji huo. 336420
captcha