Mfumo huo umezinduliwa baada ya michezo hiyo kukaguliwa na kuchunguzwa kwa makini kwa muda wa mwaka mmoja na wataalamu wa vyuo vikuu na vituo vya kidini. Wengine waliochangia katika kuufanikisha mfumo huo ni pamoja na wataalamu wa masuala ya nafsi na elimu jamii.
Sherehe za uzinduzi wa mfumo huo muhimu na wenye athari kubwa katika kulea jamii iliyo salama, zimehudhuriwa na viongozi wa serikali kutoka wizara na idara mbalimbali zinazohusika na masuala ya kijamii na utamaduni pamoja na wasanii mashuhuri wa humu nchini.338726