Kazi 240 za vitu vya kale na sanaa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu ambavyo vinadhihirisha sanaa na ustaarabu wa Kiislamu zitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Baadhi ya kazi hizo ni nakala za maandishi ya mkono za Qur’ani Tukufu, michoro ya kwenye kuta, mavazi, silaha, viyoo, panga na kadhalika.
Televisheni kubwa zimewekwa katika maonyesho hayo ambazo zinatoa taarifa juu ya historia ya utamaduni, sanaa na ustaarabu wa Kiislamu kwa lugha za Kifaransa, Kiholanzi, Kiingereza na Kijerumani.
Maonyesho hayo ambayo yalianza Jumamosi iliyopita yataendelea kwa kipindi cha wiki moja. 339405