Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Kabul, mwenyekiti wa baraza la uongozi la Harakati ya Kitaifa ya Afghanistan Mohammad Sadiq Chakry amelaani mashambulizi ya kinyama ya Israel huko Ghaza na kuyataja kuwa ni kinyume cha ubinaadamu. Chakry amezitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua madhubuti za kuwapa himaya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. Ameongeza kuwa, iwapo nchi za Kiislamu na Waislamu watatoa jibu kali, utawala wa Kizayuni wa Israel hautathubutu tena kutekeleza jinai za kinyama dhidi ya Wazayuni. Mwanasiasa huyo wa Afghanistan amesema iwapo nchi za Kiislamu na hasa za Kiarabu hazitachukua hatua za kuzuia jinai za Israeli basi suala hilo litakuwa doa jeusi katika historia ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Katika upande mwingine, Moulavi Habibullah Hesam, mwanachuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Afghanistan amesema: Ni jambo la kusikitisha kuona misimamo ya baadhi ya nchi za Kiislamu ya kutojali jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Waislamu wa Palestina. Moulavi Hesam amelaani vikali jinai za Israel na kutoa wito kwa Waislamu kote duniani kuwasaidia wananchi wasio na ulinzi wa Palestina.
Huku jamii ya kimataifa ikishindwa kuchukua hatu zozote za maana, utawala haramu wa Israel umeendeleza mashambulizi yake ya kijeshi huko Gaza, ambapo zaidi watu 400 tayari wamuawa na wengine zaidi ya 1,600 kujeruhiwa. 340225