Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina Dakta Ramadhani Abdullah Shallah amesema kuwa mashambulizi yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza na mauaji ya wakazi wa eneo hilo ni njama iliyopangwa na baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya kukamilisha mahesabu yao na harakati ya Hamas na wakazi wa Gaza.
Dakta Ramadhani Shallah amesema: Baadhi ya nchi za Kiarabu zimevuka mstari mwekundu na kutayarisha uwanja wa mashambulizi makubwa ya kijeshi ya utawala ghasibu wa Israel huko Gaza kwa kuupa ruhusa utawala huo na kunyamazia kimya jinai zake.
Kuhusu mjadala wa Misri kuwa mpatanishi katika juhudi za kukomesha mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza, Katibu Mkuu wa Jihad Islami amesema: Hakuna mwananchi yeyote wa Palestina wala Muislamu huru na mwenye mwamko atakayekubali Misri iwe mpatanishi kati ya utawala ghasibu wa Israel na harakati ya Hamas.
Ramadhani Abdullah Shallah amekosoa msimamo wa Misri kuhusu kadhia ya Palestina na mzingiro wa Wazayuni huko Gaza na akasisitiza kuwa, msimamo usiokuwa sahihi wa Cairo katika suala hilo unatishia pia usalama wa ndani wa Misri yenyewe. Amesema kuwa kusimamishwa mashambulizi ya anga za Israel huko Gaza na kukomeshwa mzingiro wa eneo hilo ndio masharti ya kuwepo mazungumzo kuhusu makubaliano mapya ya kusitisha vita kati ya utawala ghasibu wa Israel na harakati ya Hamas. 340349