IQNA

12:16 - January 18, 2009
Habari ID: 1732410

Wanachama wa Jumuiya ya Urafiki ya Kiislamu na Kiyahudi ya Ufaransa wajiuzulu

Wanachama Waislamu wa Jumuiya ya Urafiki ya Kiislamu na Kiyahudi ya Ufaransa wamejiuzulu kama alama ya malalamiko yao kutokana na kimya cha makuhani ya Kiyahudi mbele ya mauaji ya kinyama na jinai zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza dhidi ya watu wasio na hatia.

Jalul Siddiqi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Gazali ambaye pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Urafiki ya Kiislamu na Kiyahudi ya Ufaransa amesema kuwa tangu Israel ianzishe mshambulizi yake ya kinyama dhidi ya raia wa Gaza makuhani wa Kizayudi wanachama katika jumuiya hiyo hawajatoa taarifa yoyote ya kulaani jinai hizo.
Jalul Siddiqi ameashiria idadi kubwa ya wahanga wa mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza na akasema, kimya cha makuhani wa Kiyahudi wa Ufaransa mbele ya mauaji ya watoto na wanawake wasiokuwa na hatia kinasikitisha mno.
Jalul Siddiqi ameongeza kuwa, Jumuiya ya Urafiki ya Kiislamu na Kiyahudi ya Ufaransa iliundwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na maisha ya amani kati ya Waislamu na Wayahudi lakini makuhani wa Kizayuni wanachama katika jumuiya hiyo wametoa matamshi ya kibaguzi wakiyataja mashambulizi na jinai za Israel huko Gaza kuwa ni mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya maroketi ya harakati ya Hamas. 349625
captcha