Idara ya Mahusiano ya Umma ya Baraza la Mamufti wa Rissia imetangaza kuwa kitabu hicho kinakusanya ufumbuzi bora wa matatizo wanayokabiliana nayo Waislamu katika jamii ya sasa. Imesema kuwa viongozi wa kidini na wakuu wa taasisi mbalimbali za elimu wanausiwa kusoma kitabu hicho.
Kitabu hicho kimetengwa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inahusiana na aya za Quran na hadithi za Mtume (saw) na ya pili inahusu misingi ya Uislamu. 351548