IQNA

Maudhui ya 'nafasi ya uongozi katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu' kujadiliwa nchini Zambia

8:01 - January 24, 2009
Habari ID: 1734708
Maudhui ya 'nafasi ya uongozi katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu' itajadiliwa hivi karibuni katika televisheni ya ZNBC ya nchini Zambia, sambamba na kuadhimishwa mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Hayo yamesemwa na mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
Muhammad Asadi, mkuu wa kitengo hicho amesema kwamba, maudhui hiyo itakayoendelea kwa muda wa siku 10 za kuadhimisha ushindi huo, itajadiliwa katika kipindi cha meza duara, ambapo yeye atashirikiana na Ibrahim Chibamba, mwandishi wa Zambia, pamoja na Sheikh Abdallah Muwala, Mufti wa nchi hiyo katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na mapinduzi hayo.
Muhammad Asadi amesisitiza kwamba, masuala yatakayojadiliwa katika meza duara hiyo ni pamoja na historia ya Mapinduzi ya Kiislamu, mambo yaliyopelekea kupatikana ushindi wa mapinduzi hayo na nafasi ya uongozi wa Kiislamu katika kufanikisha mapinduzi hayo.
Katika mazungumzo hayo, Mufti wa Zambia atajadili nafasi na athari ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kuleta muamko miongoni mwa Waislamu ulimwenguni. 352746
captcha