IQNA

Maonyesho ya 'Palestina na mapambano katika kioo cha Sanaa' yafunguliwa nchini Syria

8:06 - January 24, 2009
Habari ID: 1734709
Maonyesho ya 'Palestina na mapambano katika kioo cha Sanaa' yamefunguliwa mjini Damascus Syria kwa udhamini wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maonyesho hayo yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa siku nane. Mkuu wa kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Syria amesema kuwa, maonyesho hayo ambayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiarabu cha Urithi wa Palestina yanafanyika sambamba na kuadhimishwa miaka 30 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Ufunguzi wa maonyesho hayo umehudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali ya Palestina Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa lengo la kutangaza mfungamano na Waislamu pamoja na mapambano ya kishujaa ya watu wa Palestina na hasa ya Ukanda wa Gaza, yanawashirikisha wasanii kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu, ambao wanaonyesha kazi na usanii wao wa kuvutia kwa watu wanaoyatembelea.
Miongoni mwa wasanii wanaoshiriki katika maonyesho hayo ni kutoka katika nchi za Palestina, Syria, Lebanon, Jordan , Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Misri, Saudi Arabia, Bahrain, Morocco, Algeria, Afghanistan, Azerbaijan, Uturuki, Cuba, Italia, Brazil, Indonesia, Ubelgiji,Marekani, Ugiriki, Ujerumani, Colombia, Uchina, Australia, Romania, Hispania na Uholanzi. 352748
captcha