IQNA

Maonyesho ya picha ya 'jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza'

8:37 - January 24, 2009
Habari ID: 1734711
Maonyesho ya picha yanayojadili jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza yamefanyika nchini Uturuki kwa udhamini na usimamizi wa Mursalin Tan, mwandishi mashuhuri wa nchi hiyo, katika mji wa Istanbul.
Kwa mujibu wa Kitengo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Uturuki, maonyesho hayo yamefanyika kwa ajili ya kuonyesha na kulalamikia jinai zilizotekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa ushirikiano wa madola makubwa ya kibeberu duniani dhidi ya Waislamu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Katika maonyesho hayo, kuna picha nyingi ambazo zinaonyesha mauaji ya umati ya kutisha yaliyotekelezwa bila huruma na Wazayuni dhidi ya watu wasio na hatia na hasa wanawake na watoto katika ukanda huo.
Maonyesho hayo vilevile yana picha ambazo zinaweka wazi namna ambavyo mauaji ya umati yamekuwa yakifanywa dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika nchi za Bosnia Herzegovina, Palestina, Lebanon, Afghanistan na Iraq.
Maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 29 Alkhamisi ijayo, na kiingilio ni bure kwa wanaotaka kuyatembelea na kujionea wenyewe kwa karibu jinai za kutisha za Wazayuni dhidi ya watoto na wanawake wa Gaza. 352601
captcha