IQNA

Mapambano ya Gaza kuchunguzwa katika vitabu

16:14 - January 24, 2009
Habari ID: 1735186
Waandishi wa weblogu nchini Iran wamemundikia barua Waziri wa Elimu wakitaka vitabu kuhusu mapambano ya watu wa Gaza viongezwe katika mitaala mashuleni.
Kundi la Waandishi Weblogu la "Fasle Intidhar", limesema, kuna haja ya vijana wa sasa na wa vizazi vijavyo kufahamishwa jina za Wazayuni maghasibu wanaoikalia Quds Tukufu kwa Mabavu.
Kundi la "Fasle Intidhar" liko katika mikakati ya kuwaunga mkono watu wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza ambao walivamiwa na Wazayuni katika vita visivyo na mlingano hata kidogo.
Wakereketwa hao wamesema kuwa kuna haja ya Waislamu wote kufahamishwa kuhusu jinai wanazotendewa Waislamu wa Palestina.
Wamesema katika barua yao hiyo kwamba kuvijulisha vizazi vijavyo kuhusu jinai za Wazayuni makatili kutaimarisha mwamko wa Kiislamu. 352786

captcha