IQNA

Kuanza mashindano ya kwanza ya kimataifa ya uchoraji kwenye ukuta mjini Makka

13:46 - January 26, 2009
Habari ID: 1735986
Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya uchoraji kwenye kuta kwa ajili ya kurembesha kuta za mji mtakatifu wa Makka yameanza kwa kuhudhuriwa na Usama bin Fadhl al-Bar, Meya wa mji huo.
Gazeti la nchi hiyo la al-Ukadh, limemnukuu meya huyo akisema katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo kwamba, wasanii wanaoshiriki katika mashindano hayo watawasilisha mabango yao kuhusiana na urithi, ustaarabu na utamaduni wa Kiislamu kuhusiana na uchoraji katika kuta za mji mtakatifu wa Makka. Amesema lengo la kuandaliwa mashindano hayo ya siku tatu ni kurembesha kuta, barabara na njia za umma katia mji huo na hatimaye kuubadilisha mji huo kuwa jumba kuu la maonyesho ya sanaa ya Kiislamu kwa mahujaji wanaozuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al-Kaaba na watalii.
Meya Fadhl al-Bar ameongeza kuwa, miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele katika mashindano hayo ni kudhihirisha sanaa ya kuvutia ya usanifu majengo ya Kiislamu katika karne tofauti, kuchorwa maeneo ya maumbile ya asilia na ya kidini ya Makka na vilevile michoro tofauti ya Kiarabu.
Meya al-Bar amesema mwishoni mwa matamshi yake kwamba, washindi wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi nono kwa ajili ya kuwapa moyo wa kushiriki katika mashindano mbalimbali ya sanaa ya Kiislamu kwa madhumuni ya kurembesha mji mtakatifu wa Makka kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu.353749
captcha