Sherehe za kuenziwa watu hao ambazo zimeandaliwa na Taasisi ya Qur'ani Tukufu zitafanyika tarehe 18 Februari katika ukumbi wa Sheikh Swaduq katika haramu la Abdul Adhim Hassani. Mbali na kutunukiwa zawadi wachapishaji watatu mashuhuri wa Qur'ani na muhifadhi mmoja wa kitabu hicho kitakatifu, watu wengine watakaoenziwa katika kikao hicho ni pamoja na watayarishaji wa duru ya tatu ya mpango wa kutathmini na kutoa vyeti maalumu kwa wahifadhi na washindi bora wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika mwaka huu wa Kiirani.
Kundi hilo litasaidiwa kulipa gharama ya kufanya umra katika mji mtakatifu wa Makka.
Sherehe hizo zitaanza mara tu baada ya kumalizika swala ya Maghrib na Ishaa tarehe iliyotajwa. 354069