IQNA

Mkutano wa Uislamu na Ubuddha nchini Thailand

13:42 - January 27, 2009
Habari ID: 1736449
Mkutano wa Uislamu na Ubuddha unatazamiwa kufanyika tarehe 6 Februari katika Chuo Kikuu cha Mahachulalongkomrajavidyalata nchini Thailand. Mkutano huo utasimamia na chuo hicho na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand.
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran huko Thailand amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, utajadili masuala yanazikutanisha pamoja dini mbili za Uislamu na Ubuddha na uhusiano wa kihistoria na kitamaduni wa Iran na Thailand ambao una historia ya zaidi ya miaka mia nne.
Mkutano huo utahudhuriwa na Wasomi, wanafikra wa vyuo vikuu na wataalamu wa masuala ya kidini.
Ujumbe wa Iran katika mkutano huo utaongozwa na Mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni na mawasiliano ya Kiislamu Mahdi Mustafavi. 354277
captcha