Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini China kimetangaza kwamba mashindano hayo yatahusisha sekta ya mashairi, uandishi wa kumbukumbu na historia ya Mapinduzi ya Kiislamu kwa Wairani waishio China.
Mashindano hayo pia yatafanyika sambamba na ufunguzi wa kituo cha utafiti wa masuala ya Iran katika Akademia ya Elimu Jamii kwenye mkoa unaojiendeshea mambo yake wa Ningxia.
Kituo hicho kinafunguliwa kwa lengo la kutoa nafasi za masomo, kubadilishana wahadhiri na walimu, kuitishwa semina za kielimu na kwa ajili ya kufanya uhakiki wa pamoja kati ya China na Iran.
Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Iran katika mkoa wa Ningxia kitakuwa kikifanya kazi wakati wote na kitashughulikia pia masuala ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kidini. 354335