IQNA

Jumba la makumbusho la Qatar ni dhihiriso la kunawiri ustaarabu wa Kiislamu

15:26 - January 27, 2009
Habari ID: 1736567
Waziri Mkuu wa Hungary Ferentsem Dyurchanem ametembelea jengo la makumbusho la Sanaa za Kiisalmu nchini Qatar na kusema athari za sanaa zilizopo katika jumba hilo ni dhihirisho la kunawiri ustaarabu na utamaduni wa Kiislamu katika zama tofauti.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qatar (QNA), baada ya Dyurchanem kutembelea jengo hilo la makumbusho mjini Doha amesema kuwa: “Athari na vifaa vya sanaa katika jengo la makumbusho la Doha ni vyenye thamani kubwa na viashirio vya kunawiri na kustawi Waislamu katika zama tafauti”.
Ameongeza kuwa hatua ya Qatar ya kukusanya athari za sanaa za Kiislamu kutoka nchi zote za ulimwengu wa Kiislamu katika Jumba la Makumbusho la Sanaa ya Kiislamu mjini Doha itastawisha mazungumzo na mabadilishano ya kiutamaduni.
Waziri Mkuu wa Hungary na ujumbe wake aliwasili Qatar Jumatatu iliyopita kwa lengo la kujadili njia za kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili na vile vile kutathmini matukio ya kimataifa.
Katika Jumba la Makumbusho la Sanaa ya Kiislamu mjini Doha kuna athari mbalimbali za sanaa zilizokusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu katika karne tofauti. Mjumuiko huo wa athari za sanaa ni wa aina yake duniani. 354532
captcha