IQNA

Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu yaanza Afrika Kusini

11:30 - February 01, 2009
Habari ID: 1738281
Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu imeanza katika mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini ikisimamiwa na Kamati ya Utendaji ya Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu katika nchi mbalimbali za Kiislamu kwa kushirikiana na baraza la mji wa Pretoria.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ismail Abedi Aal Ali amesema kuwa katika wiki hiyo kutafanyika maonyesho ya picha za turathi za kihistoria, misikiti na vituo vya kidini katika nchi mbalimbali za Kiislamu.
Amesema kuwa, vilevile kutakuwepo maonyesho ya sanaa ya Kiislamu na sana za kutengeneza kwa mkono pamoja na michezo ya kuigiza itakayohusu mila na desturi za Kiislamu, maonyesho ya filamu za matukio ya kweli (documentary) za maeneo ya kidini ya Makka, Madina na msikiti wa al Aqsa.
Ismail Aal Abedi amesema kuwa uhusiano wa nchi za Kiislamu na Afrika ulianza katika karne ya saba Miladia na kwamba nchi za Kiislamu ziliunga mkono harakati za ukombozi na kupigania uhuru za Afrika Kusini. Amesisitiza kuwa uhusiano wa Afrika Kusini na nchi za Kiarabu na Kiislamu unaimarika zaidi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kitamaduni, kijamii, kibiashara na kiuchumi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu ameongeza kuwa kufanyika kwa wiki ya Kiutamaduni ya Kiislamu ni hatua muhimu katika njia ya kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na fursa nzuri ya wananchi wa Afrika Kusini kutambua utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu.
Sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu katika mji wa Pretoria zilihudhuriwa na mabalozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu nchini Afrika Kusini. 356701
captcha