IQNA

Kitabu cha "Demokrasia ya Kidini" chachapishwa nchini Russia

11:12 - February 01, 2009
Habari ID: 1738452
Kitabu cha "Demokrasia ya Kidini, Hakika, Maana na Maswali ya Kisiasa" kimechapishwa katika mji wa Saint Petersburg nchini Russia.
Kitabu hicho ambacho kimechapishwa kwa hisani ya Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Russia na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kiutamaduni na Kimataifa cha Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu nchini Iran, kinakusanya makala zilizowasilishwa katika mkutano wa "Demokrasia ya Kidini, Zama za Sasa na Mustakbali wa Ulimwengu wa Kiislamu".
Sehemu nyingine ya kitabu hicho inazungumzia demokrasia ya kidini nchini Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kitabu cha Demokrasia ya Kidini ambacho kina kurasa 424 kimechapishwa kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 30 ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. 356376
captcha