IQNA

Maonyesho ya kimataifa ya Msikamano na Watoto wa Gaza

11:11 - February 01, 2009
Habari ID: 1738456
Maonyesho ya kimataifa ya Mfungamano na Watoto wa Ukanda wa Gaza yamenza mjini Muscat, Oman.
Wasanii kutoka nchi za Sudan, Jordan, Syria, Oman na Iraq wanashiriki katika maonyesho hayo. Mabango 48 ya sanaa ya uchoraji yanayohusu maudhui ya mshikamano na watoto wa Gaza yanaonyeshwa katika maonyesho ya Muscat.
Mkurugenzi wa maonyesho hayo Abdulrauf Sham'un amesema kuwa mauaji yaliyofanywa dhidi ya watoto wadogo wa Ukanda wa Gaza, mashaka ya wakazi wa eneo hilo baada ya mashambulizi ya siku 22 ya utawala ghasibu wa Israel, kuharibiwa kwa nyumba na miundombinu ya Gaza, kusimama kidete Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na wananchi wa Gaza mbele ya jinai za Wazayuni ni miongoni mwa maudhui zinazoonyeshwa kwenye mabango ya wasanii wanaoshiriki kwenye maonyesho hayo.
Msanii Jihad al A'miri wa Jordan amesema kuwa maonyesho ya kazi hizo za kisanii ni hatua ya kitamaduni ya kukabiliana na ukatili wa Wazayuni na mauaji yao huko Gaza. Ameongeza kuwa wananchi wa Gaza hawahitaji misaada ya chakula na dawa pekee, bali wasanii wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wanapaswa kupongeza mapambano ya kishujaa ya watu wa Gaza kwa kutunga mashairi, nyimbo na kufanya maonyesho ya kazi za sanaa.
Maonyesho ya sanaa ya msikamano na watoto wa Gaza mjini Muscat ambayo yalianza Ijumaa iliyopita yataendelea hadi Jumatano ya wiki hii. 356719
captcha