IQNA

Wanaharakati wa habari za Ashura waenziwa Uturuki

13:59 - February 02, 2009
Habari ID: 1738980
Waandishi habari waliohusika katika kupasha habari za siku ya Ashura nchini Uturuki wameenziwa kwa jitihada zao muhimu.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Khema, Taasisi ya Ja’afari ya Uturuki imeandaa sherehe maalumu na kuwatunuku zawadi waandishi habari wakiwemo, wapiga picha, maripota na watayarishaji vipindi vya radio na televisheni na vile vile waandishi magazeti kwa jitihada zao za kuakisi ipasavyo shughuli za siku ya Ashura nchini Uturuki.
Kiongozi wa Mashia wa Uturuki amesema, siku ya Ashura ni siku ya kuomboleza kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume (saw), Imam Hussein AS.
Salahdin Uzrugunduz ameongeza kuwa kuna baadhi ya riwaya zisizo za kweli zinazojaribu kupotosha fikra za umma kuhusu tukio la Ashura. Amezitaja hadithi kama hizo kuwa ni hadithi za Kiisraili na zilizobuniwa na viongozi wa Bani Umayyah.
Amesema, baadhi ya hadithi hizo potofu zimechapishwa katika Encyclopedia ya Shirika la Masuala ya Kidini la Uturuki na ametaka shirika hilo kurekebisha makosa hayo.
Salahdin Uzrugunduz amesema, katika miaka ya hivi karibuni vyombo vya habari vya Uturuki vimekuwa vikiipa umuhimu siku ya Ashura na kuongeza kuwa kuna haja ya kuakisi habari sahihi kuhusu siku ya Ashura na kuepuka kutoa habari za upotoshaji wa tukio hili muhimu la Kiislamu. 357483

captcha