IQNA

Mafunzo ya muda ya fikra za Kiislamu katika Kituo cha Kiislamu Uingereza

13:19 - February 02, 2009
Habari ID: 1739016
Mafunzo ya muda ya fikra za Kiislamu yameanza katika Kituo cha Kiislamu cha Uingereza na yanatazamiwa kuendelea hadi mapema mwezi Aprili.
Mafunzo hayo ya muda yatahusu elimu ya misingi ya dini, historia ya Kiislamu, utafiti wa Qur'ani, masuala ya kiroho ya Kiislamu na masuala ya sasa.
Mafunzo hayo yalianza jana kwa kuchunguza historia ya maisha ya Nabii Muhammad (saw) tangu kuzaliwa kwake hadi kuaga dunia na kipindi cha serikali za makhalifa wanne hadi wakati wa kuuawa shahidi Imam Ali bin Abu Twalib (as).
Mishoni mwa mafunzo hayo ya muda washiriki watatunukiwa shahada maalumu. 357315

captcha