IQNA

Kufanyika maonyesho ya hati za Iran katika nchi 10 duniani

9:15 - February 03, 2009
Habari ID: 1739435
Maonyesho ya "Chaguo bora la hati za Kiirani" yanayojumuisha taswira zenye thamani kubwa za hati za Iran zinazohifadhiwa katika Maktaba ya Kitaifa ya Iran kwa mara ya kwanza zitaonyeshwa nje ya nchi kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Maktaba ya Kitaifa, maonyesho hayo yatafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Taifa ya Nyaraka na Maktaba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Idara ya Maadhimisho ya Mwaka wa 30 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na balozi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi za Austria, Jamhuri ya Kyrgyzstan, Australia, China, Oman, Lebanon, Jamhuri ya Belarus, Vatican na Jamhuri ya Czech.
Maonyesho hayo yanafanyika kufuatia safari ya Ali Akbar Ash'ari Mshauri wa Utamaduni wa Rais wa nchi ambaye pia ni Mkuu Taasisi Kitaifa ya Nyaraka na Maktaba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi kunakofanyika maonyesho hayo.
Kati ya athari 40 zitakazoonyshwa katika nchi hizo ni nuskha za hazi za diwani za Hafiz Shirazi, Saadi, Mathnawi Maanawi, Nukhbar Khawrzmshahi, Miniature, nyaraka za Behzad na michoro iitwayo Jalalahu Allah ya Mohammad Ahsâ’i. Baada ya kumalizika maonyesho kazi hizo za sanaa zitakabidhiwa kwa maktaba za kitaifa za nchi wenyeji. 358176
captcha