Kwa msimamo wake wa kishujaa katika kuwatetea wananchi wa Ukanda wa Gaza na kutoa matamshi ya fahari katika kulaani jinai za kivita za Wazayuni dhidi ya watoto wadogo na wanawake wasio na hatia wa ukanda huo, Rajab Tayyib Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki, ameimarisha moyo wa wapigania haki ulimwenguni na hivyo kuwa mtetezi halisi wa haki za wakazi wa Gaza badala ya wale wanaotoa madai matupu eti ya kueteta haki za binadamu duniani.
Hayo yamesemwa na Harakati ya Maulamaa wa al-Azhar ambao wametoa taarifa wakisifu msimamo wa kishujaa wa Erdogan katika kutoa jibu kali kwa madai na propaganda tupu za Shimon Peres, Rais wa utawala haramu wa Israel katika jukwa la masuala ya kiuchumi huko Davos Uswisi, aliyejaribu kuhalalisha hujuma ya Wazayuni dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza.
Maulama hao wamesema katika taarifa yao kwamba, mapokezi makubwa ya wananchi wa Uturuki kwa Waziri Mkuu wao yameufurahisha mno umma mzima wa Kiislamu na nchi za Kiarabu na hivyo kudhihirisha thamani kubwa ya msimamo huo wa Waziri Mkuu Erdogan katika kulalamikia jinai hizo za Wazayuni dhidi ya watu wasio na hatia na uongo wa Peres wa kujaribu kuhalalisha jinai hizo. Wamesema hatua hiyo ya Erdogan inabainishja wazi siasa za ubaguzi wa rangi za utawala wa Israel, ambazo zimezusha hasira kubwa ulimwenguni dhidi ya Israel. Taarifa hiyo imesema kuwa, hatua hiyo ya Erdogan ambayo imehuisha moyo wa kupigania uhuru miongoni mwa Wapalestina, kamwe haitasahaulika na wapigania uhuru ulimwenguni. 358009