Masuala mbalimbali ya maisha ya Imam Kadhim (as) katika kivuli cha Qur'ani na siasa za kiuadui za watawala wa Bani Abbas dhidi yake yamejadiliwa katika toleo hilo.
Mafundisho ya kimalezi ya Imam Kadhim, urithi na kuuawa kwake shahidi, mapambano na hadithi zake ni mambo mengine ambayo yamejadiliwa katika toleo hilo. Siku ya kuzaliwa Imam huyo wa saba wa Waislamu wa Kishia, yaani Jumapili tarehe 7 Swafar 128 Hijiria kulisadifiana na miaka ya mwisho ya ukhalifa wa Mansur Abbasi.
Imam Musa Kadhim alipata uimamu kutoka kwa baba yake akiwa na umri wa miaka 21 kutokana na hali maalumu iliyokuwa ikitawala katika kipindi hicho, na kuendelea kuwa Imamu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 35. Kipindi hicho cha uimamu wake kilikuwa kirefu zaidi kuliko Maimamu wengine wote, isipokuwa Imam wa Zama (af).
Miongoni mwa sifa na mambo aliyojishughulisha nayo sana mtukufu huyo ni kuhusiana na suala la malezi ya watoto kwa ajili ya kulea jamii iliyosalimika na safi inayozingatia thamani za ubinadamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu. 359290