IQNA

Tamasha ya kimataifa ya filamu za Kiislamu kufanyika Washington

11:30 - February 05, 2009
Habari ID: 1740483
Tamasha ya pili ya kimataifa ya filamu za Kiislamu itafanyika tarehe 13 Februari hadi 12 Machi mwaka huu mjini Washington, Marekani.
Kituo cha Muslimfilm kimeripoti kuwa katika tamasha hiyo filamu za wasanii wa Kiislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia zitakazojadili maudhui ya "Sanaa Katika Moto" zitakaribishwa katika vyuo vikuu vitano vya America, George Town, George Washington, George Mison na Marriland.
Lengo la Tamasha hilo litakalosimamiwa na Baraza la Kiislamu la Marekani ni kuchunguza tofauti za kiutamaduni na kifikra za Waislamu kote duniani na kueneza fikra ya uvumilivu na mazungumzo kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Baraza la Kiislamu la Marekani (AIC) ni taasisi isiyokuwa ya serikali ambayo iliasisiwa mwaka 2001 na Waislamu wa Marekani kwa lengo la kueneza fikra ya kuvumiliana na maelewano kati ya wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali. Ofisi kuu za taasisi hiyo iko mjini Washington na ina matawi katika miji ya Boston, Cairo na Basra huko Iraq. 359318

captcha