IQNA

Kususiwa filamu iliyo dhidi ya Uislamu nchini Indonesia

10:44 - February 07, 2009
Habari ID: 1741051
Mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini Indonesia ametoa wito wa kususiwa filamu inayoitwa, 'Mwanamke Mwenye Mtandio Shingoni.'
Gazeti la nchi hiyo la News limemnukuu Ali Mustafa Ya'qub Imamu wa 'Msikiti wa Kujitawala' mjini Jakarta akisema kuwa, licha ya kuwa filamu hiyo inaukosea heshima Uislamu, inapotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mtazamo adilifu wa dini tukufu ya Kiislamu kuhusiana na mwanamke.
Ya'qub ameendelea kusema kuwa, picha inayotolewa na filamu hiyo ya kibaguzi kuhusiana na Uislamu na vituo vya kielimu vya Kiislamu ni ya kupotosha kabisa, ya kusikitisha na ya dharau moja kwa moja dhidi ya Uislamu. Ameseme, kwa mtazamo wake filamu hiyo inapasa kususiwa na Waislamu wote.
Kisa cha filamu hiyo kinahusiana na maisha ya binti mmoja wa Kiislamu ambaye baba yake mzazi ni mwanazuoni anayezingatia sana masuala ya kidini. Binti huyo anapinga vikali vikwazo vya shule yake ya Kiislamu inayoendesha shughuli zake usiku na mchana. 360268
captcha