Hayo yamesemwa na Azizullah Haji Mash'hadi, mkosoaji na mwalimu wa filamu nchini Iran, katika Tamasha ya Filamu ya Fajr mjini Tehran. Amesema kuwa sekta ya filamu ya Magharibi hususan Marekani, inafanya jitihada za kuwa na mtazamo hasi kuhusu Mashariki na Uislamu kutokana na kudhibitiwa na fikra za Kizayuni.
Akijibu swali kwamba, Je, fikra na mtazamo huo unaongozwa na wanasiasa? Haji Mash'hadi amesema: Wanasiasa wa nchi za Magharibi ndio wanaoainisha stratijia ya utamaduni na sanaa. "Wasanii wakitaka kutengeneza filamu za kitaifa huchukua sera na miongozo kutoka kwa wanasiasa na kwa sababu hiyo hatuwezi kukana nafasi ya wanasiasa katika uwanja huo", amesisitiza mkosoaji huyo wa filamu.
Amesema kuwa inasikitisha kwamba kutokana na kuwa ulimwengu wa Kiislamu au jamii na mataifa ya Kiislamu au wasanii Waislamu hawatengenezi filamu za kuwaelimisha watu kidini au kwa uchache hawatilii maanani suala hilo kwa kiwango cha kutosha, fikra za waliowengi dunaini hususan Wamagharibi wanaelekea kukubali uchambuzi wa mtazamo hasi wa filamu za Magharibi kuhusu Uislamu.
Amezitaka tasisi mbalimbali za Kiislamu kushirikiana na kutengeneza filamu zinazokidhi matakwa ya zama za sasa. 360478