Mtayarishaji wa filamu hiyo Atif Issa amesema kuwa utengenezaji wa filamu hiyo utaanza hivi karibuni na kusajili maafa ya kusikitisha ya watu wa Gaza.
Amesema kuwa filamu hiyo itatengenezwa na mashirika mawili ya Palestina na Ufaransa na kwamba itaonyesha unyama na ukatili wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 22 huko Gaza.
Atif Issa amesisitiza kuwa filamu hiyo itatengenezwa kwa lugha nne za Kifaransa, Kiingereza, Kiarabu na Kiturki na kwamba utengenezaji wake utadumu kwa kipindi cha wiki saba. Ameongeza kuwa baadhi ya vipengee vya filamu hiyo vilitayarishwa wakati wa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema: Kanali nyingi za televisheni duniani zinataka kuonyesha filamu hiyo.
Atif Issa amesema kuwa filamu hiyo itakuwa na sehemu mbili ambazo kila sehemu yake moja inachukua muda wa dakika 45. Amesema kuwa sehemu ya kwanza ya filamu hiyo itahusu mashaka na masaibu ya wakazi wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel dhidi ya eneo hilo na sehemu ya pili itagusia matatizo ya waandishi habari waliokuwa wakiripoti matukio mbalimbali na mashambulizi ya anga ya Israel katika eneo hlo. 360583