IQNA

Kuanza mashindano ya kuhifadhi hadithi za Mtume (saw) nchini Imarati

22:42 - February 08, 2009
Habari ID: 1741705
Duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi hadithi za Mtume (saw) ilianza Jumamosi iliyopita nchini Imarati katika Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Abu Dhabi, mji mkuu wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Khaleej, Katibu wa mashindano hayo Ali bin Jabir Elhamli amesema, mashindao hayo yanafanyika ufadhili wa Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Abu Dhabi na usimamizi wa Idara ya Waqfu na Masuala ya Kiisalmu ya Imarati.
Ameongeza kuwa, mashindayo hayo yatakuwa na washiriki 650 watakaojumuisha wanaume na wanawake. Kuna viwango vya wale waliohifadhi hadithi, 150, 125, 100, 60 na 40.
Ali bin Jabir Elhamli amesema kuwa duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi hadithi za Mtume Muhammad (saw) nchini Imarati itaendelea kwa siku tatu na watakaofuzu watapewa zawadi na chetu cha shukrani. 360418

captcha