Tovuti ya KashmirWatch imeandika kuwa, mara tu baada ya kuenea habari hiyo, Waislamu wa Kashmir walikusanyika katika eneo hilo na kulalamikia vikali jambo hilo.
Baada ya kushuhudia mkusanyiko huo mkubwa wa Waislamu, polisi ilimkamata mtalii huyo mara moja na kumsaili kuhusiana na jambo hilo.
Baada ya mahojiano, mtalii huyo alisema kuwa mkewe ambaye ni raia wa Qatar siku chache zilizopita alimpa vipachiko ambavyo vilikuwa vimeandikwa juu yake aya za Qur’ani Tukufu naye akaamua kuvibandika kwenye relitheluji hizo bila ya kutambua athari na matokeo yake. 361379