IQNA

Mshauri wa Rais Ahmadinejad akutana na mkuu wa baraza la utamaduni la India

18:41 - February 12, 2009
Habari ID: 1743193
Mahdi Mustafavi Mshauri wa Rais Ahmadinejad wa Iran ambaye pia ni mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu amekutana na Karan Singh Mkuu wa Baraza la Utamaduni la India na wamejadili suala la kuimarishwa uhusiano wa kiutamaduni kati ya pande hizo mbili.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini India, maafisa hao wawili walijadili pia suala la maandalizi ya Wiki ya Utamaduni nchini India na vilevile kuanzishwa vitengo vya lugha ya Kifarsi na masuala ya Iran katika vyo vikuu vya India.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Balozi wa Iran nchini India Sayyid Mahdi Nabizadeh na Karim Najafi Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini humo.
Mwishoni mwa mkutano huo pande mbili ziliafikiana kuwa India na Iran zitatia saini mapatano katika masuala ya utamaduni na sanaa.
Mahdi Mustafavi Mshauri wa Rais Ahmadinejad wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu yuko safarini nchini India na ametembelea maeneo mbalimbali na kukutana na maafasi wa ngazi za juu wa utamaduni nchini humo. 362442
captcha