IQNA

12:27 - February 14, 2009
Habari ID: 1743622

Qur'ani Tukufu kwa mara ya kwanza itatarjumiwa katika lugha ya ishara

Kwa mara ya kwanza kabisa watarjumi na watafiti wa Qur'anii Tukufu katika Taasisi ya Qur'ani ya Mfalme Fahd katika mji mtakatifu wa Madina wamejiandaa kutarjumu kitabu hiki kitakatifu katika lugha ya ishara.

Gazeti la Saudi Arabia la al-Madina limemnukuu Muhammad Salim bin Shadid al-Aufi akisema kuwa taasisi hiyo imechukua hatua muhimu za mwanzo za kutarjumu kitabu hicho katika lugha ya ishara na kwamba hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa hatua kama hiyo kuchukuliwa duniani. Ameongeza kwamba, Taasisi ya Qur'ani ya Mfalme Fahd itatoa suhula zote za kiufundi na kitaaluma kwa ajili ya kuwawezesha watarjumi na watafiti wa Qur'ani kutarjumu kitabu hicho kitakatifu katika lugha ya ishara, kazi ambayo amesisitiza kwamba itaanza hivi karibuni katika taasisi hiyo.
Al-Aufi ameongeza kwamba, taasisi hiyo huchapisha kila mwaka karibu kopi milioni kumi za Qur'ani katika lugha tofauti. Amesema kufikia mwaka jana, taasisi hiyo ilikuwa imechapisha anwani 230 za vitabu mbalimbali, ikiwemo tarjuma ya Qur'ani katika lugha tofauti, vitabu kuhusiana na sira na Sunna za Mtume (saw), tarjuma za juzuu tofauti za Qur'ani na kanda za sauti na picha mbalimbali za Kiislamu. 363359
captcha