IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Hollywood zinatokana na wasimamizi wake wa Kizayuni

12:45 - February 15, 2009
Habari ID: 1744181
Sababu ya filamu za Hollywood kuwa na mitazami iliyo dhidi ya Uislamu ni kuwa taasisi hiyo ya utengenezaji filamu inasimamiwa na Wazyauni; wa msingi huo haipaswi kutarajia chombo hicho kuwa na mtazamo mzuru kuhusu Uislamu.
Arash Sajjadi Husseini mtaalamu wa masuala ya filamu amezungumzia kuhusu sera zinazotumiwa katika filamu za Hollywood na kusema: "Sababu ya filamu za Magharibi hasa Hollywood kutoa maana potofu na zinazouvunjia heshima Uislamu ni sisi Waislamu kutofanya juhudi za kutosha katika sekta ya utengenezaji filamu kimataifa ili kubainisha sura halisi na thamani za Uislamu kwa walimwengu".
Mtaalamu huyo wa masuala ya filamu amesema kuwa, chuki dhidi ya Uislamu katika filamu za kimataifa ilianza miaka kadhaa iliyopita. Arash Sajjadi Husseini amesema, filamu zilizo dhidi ya Uislamu zina watazamaji wake maalumu.
Mweledi huyo wa falamu wa Iran anasema, Waislamu wanapaswa kuchukua hatua imara za kukabiliana na fialmu potofu za Hollywood. Amesema kuwa kuna haja ya kutengeneza idadi kubwa ya filamu ambazo zitaonyesha thamani za Kiislamu kwa mitazamo mbalimbali. Ameongeza kuwa mbali na idadi kubwa ya filamu suala la ubora linapaswa pia kuzingatiwa ili kazi zitakazotayarishwa ziweze kudumu na kuwa na taathira inayotakikana. Pia filamu za ustaarabu wa Kiislamu zinapaswa kuvutia hisia za watazamaji ili ziweze kufikisha ujumbe. 363895
captcha