Ibrahim Muhammad Bumulihha, mkuu wa kamati inayosimamia mashindano hayo anasema kuwa, mashindano hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa taasisi za Kiislamu na mashirika ya vyombo vya habari na magazeti muhimu ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Amesema, mashindano hayo yanafanyika katika makundi mawili ya wanaume na wanawake na kwamba yanafanyika kwa uungaji mkono na msaada wa Muhammad bin Rashid Aal Maktum, mtawala wa Dubai na kwa ushirikiano wa Taasisi ya Zawadi ya Qur'ani ya Dubai.
Bumulihha amesema kuwa, kwa kuzingatia ukaribisho mkubwa ambao umeonyeshwa na wapenzi wa Qur'ani kwa mashindano hayo, kamati inayosimamia mashindano hayo imesema kuwa, wasimamizi pia wataandaa mashindano ya kuhifadhi juzuu tatu za Qur'ani maalumu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi. Amesema, nyanja za kusoma na kuhifadhi Qur'ani nzima zimeongezwa katika mashindano ya zawadi hiyo ya Dubai.
Mkuu huyo wa zawadi ya Dubai amemalizia kwa kusema, hatua za mwanzo za mashindano hayo zilifanyika awali katika miji ya Dubai, Abu Dhabi, Sharjah, Ras al-Kheimah, Ajman, Ummu Qawiyain na al-Ain huko Imarati.
Washindani walioshinda katika hatua hiyo ndio waliofanikiwa kushiriki katika hatua hii ya pili na ya mwisho ya mashindano ya Zawadi ya Dubai. 363727