IQNA

14:35 - February 16, 2009
Habari ID: 1744670

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa yalaani mauaji dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (as)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetoa taarifa ikilaani hatua ya kinyama ya mauaji yaliyotokelezwa hivi karibuni na magaidi dhidi ya waombolezaji wa Arbaini ya Imam Hussein (as) huko nchini Iraq.

Katika taarifa hiyo, Bernard Kouchner, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa amelaani vikali hatua hiyo ya makundi ya kigaidi yenye misimamo ya kupindukia mipaka dhidi ya waombolezaji waliokuwa njiani kuelekea Karbala kwa ajili ya kushiriki katika marasimu ya Arbaini ya Imam Hussein (as).
Taarifa hiyo imesisitiza kwamba, serikali ya Ufaransa ingali inaunga mkono na itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya hivi sasa ya Iraq kwa ajili ya kurudisha amani na utulivu katika nchi hiyo na kwamba itafanya juhudi kuhakikisha kwamba lengo hilo linafikiwa.
Siku ya Ijumaa, kundi moja la Waislamu wa Kishia waliokuwa njiani wakitembea kwa miguu ili kushiriki katika maombolezo hayo ambayo yanafikia kilele leo Jumatatu, lililengwa na magaidi huko kusini mwa Baghdad ambao walilipua bomu lililopelekea karibu watu 40 kupoteza maisha yao na wengine 80 kujeruhiwa. 364470
captcha