IQNA

Tamasha ya kwanza ya filamu za masuala ya kibinadamu kufanyika mjini Tehran

11:26 - February 18, 2009
Habari ID: 1745462
Tamasha ya kwanza ya kimataifa ya filamu za masuala ya kibinadamu inatazamiwa kufanyika tarehe 27 Aprili mpaka Mei Mosi mwaka huu mjini Tehran ikihudhuriwa na watengenezaji filamu mashuhuri wa nchi mbalimbali.
Kamati ya upashaji habari ya tamasha hiyo ya filamu za masuala ya kibinadamu imetangaza kuwa Baraza Kuu la tamasha hilo linajumuisha shakhsia kadhaa wenye uzoefu katika medani hiyo.
Lengo la tamasha hiyo ni kutumia uwezo wa watengeneza filamu na sanaa hiyo katika masuala ya kibinadamu, kuanzisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na kutayarisha uwanja wa kueneza mitazamo na fikra za kisasa kuhusu mahusiano ya shughuli za kibinadamu. 365464

captcha