IQNA

Mtazamo wa Hollywood kuhusu Uislamu ni wa kisiasa

12:27 - February 19, 2009
Habari ID: 1745938
Mtazamo wa filamu za Magharibi na hasa Hollywood kuhusu Uislamu ni wa kisiasa kabisa.
Akizungmza na IQNA, Shahriyar Asadi, mtengeneza filamu wa Iran amesema kuwa filamu kama hizo zinazotengenezwa kwa malengo ya kupotosha haziweza kuacha athari za kudumu miongoni mwa watazamaji. Amesema yamkini watazamaji wakaathiriwa wakiwa ndani ya ukumbi wa sinema, lakini baada ya muda uhakika huweza kuwabainikia.
Assadi amesema watengeneza fialmu wa Iran kinyume na wenzao wa Magharibi, hawalengi hata kidogo kuvunjia heshima matukufu ya dini za wengine.
Amesema ili kuhakikisha filamu zilizo dhidi ya Uislamu za Wamagharibi haziachi athari zozote, kuna umuhimu wa kutengenezwa filamu zinazouarifisha Uislamu ili walimwengu waweze kuufahamu Uislamu halisi. 365914
captcha