IQNA

Vitabu kuhusu Uislamu na Qur'ani chachapishwa Ufaransa

12:35 - February 19, 2009
Habari ID: 1745943
Vitabu 12 kuhusu Qur'ani Tukufu, Mtume Mtukufu (SAW), Nahjul Balagha na Imam Hussein (AS) vimechapishwa kwa hisani ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ufaransa.
Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ufaransa imesema vitabu vilivyochapiswa ni: "Qur'ani, Kitabu cha Muongozo" cha Ali Reza Muradi "Ukweli Kuhusu Waliomrithi Mtume (SAW)" kilichoandikwa na Muhammad Ali Haidar, "Hizbullah, Mbinu, Uzoefu na Mustaqabali" kilichoandiwa na Sheikh Naem Qasim, "Siri ya Sala" kilichoandikwa na Imam Khomeini (MA), na "Athari na Sababu za Mapinduzi ya Imam Hussein (AS)" kilichoandikwa na Shahid Muttahari.
Vitabu vingine vilivyochapishwa na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Ufaransa ni: "Mtume (SAW) na Sunna ya Utume" kilichoandikwa na Sayyed Hussein Nasser, "Mahdi, Hakimu wa Dunia" kilichoandikwa na Ayatullah Amini, "Hadithi Arobaini" cha Imam Khomeini (MA) na "Risala ya Haki za Binaadamu ya Imam Sajjad (AS)" na "Encyclopedia ya Wasomi wa Kiirani" kilicoandikwa na Mashid Mushiri. 366103
captcha