IQNA

Toleo jipya la "Iran ya Kitamaduni" latangazwa Lebanon

12:13 - February 19, 2009
Habari ID: 1745973
Toleo jipya la jarida la kila miezi mitatu la "Iran ya Kitamaduni" limechapishwa nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, jarida hilo lina makala mbalimbali kuhusu turathi za kiutamaduni na sanaa ya Iran. Jarida hilo lina makala kama vile: "Iran ya Kiisalmu na Suala la Post Modernism" iliyoandikwa na Muhammad Haidar wa Lebanon.
Jarida hilo pia lina makala kuhusu athari za kihistoria na kidini katika mji mtakatifu wa Mash'had na utafiti kuhusu mwanafalsafa maarufu Muirani Abu Ali Sina. Aidha jarida hilo lina makala za kitaalamu zinazojadili nadharia za Imam Khomeini kuhusu utamaduni wa taifa na utawala.
Tahariri ya toleo jipya la jarida la "Iran ya Kitamaduni" ina anwani isemayo: "Mazungumzo baina ya utamaduni na kuhifadhi anuai". Tahariri hiyo imeandikwa na Muhammad Said ambaye anajadili muhimu wa mazungumzo katika kutengeneza daraka za mawasiliano baina ya staarabu za mwanadamu hasa ustaarabu wa Kiisalmu. 365967
captcha