IQNA

Wasaudia waharibu turathi za kihistoria za Kiislamu kwa kisingizio cha kupambana na ushirikina

12:33 - February 21, 2009
Habari ID: 1746622
Mwanazuoni mmoja mashuhuri wa Saudi Arabia amekemea juhudi zinazofanywa na viongozi na baadhi ya wanazuoni wa kidini nchini humo za kuharibu maeneo ya kihistoria ya Kiislamu kwa kisingizio cha kupambana na ushirikiana.
Shirika la habari la kimataifa la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu IINA limeripoti kuwa Sheikh Abdulmuhsin al Abikan ambaye ni Mshauri wa Mfalme wa Saudi Arabia, amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa turathi za kihistoria za Kiislamu nchini humo.
al Abikan ametoa pendekezo la kuzidishwa kikosi maalumu cha polisi katika maeneo ya kihistoria ya Kiislamu ili kuzuia alichodai ni vitendo vya ushirikina badala ya kuyavunja maeneo hayo.
Tangu walipochukua madaraka nchini Saudi Arabia, Mawahabi wenye misimamo mikali ya kidini na chuki za kimadhehebu wamekuwa wakiharibu athari za kihistoria za Kiislamu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina kwa kisingizio cha kupambana na opotofu na ushirikina. Kundi hilo linafanya njama za kuharibu maeneo ya kihistoria na kidini yaliyosalia hadi hivi sasa. 366746

captcha